February 15, 2013
Mwendeshaji
wa Kipindi cha Ongea na Janet kinachorusshwa na Clouds Tv na DStv
Channel 158 Bi. Janet Sosthenes Mwenda akisaini daftari la wageni katika
kituo cha kulelea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kiwohede
kilichopo Buguruni jijini Dar es Salaam mara baada ya kuwasili kwa
ajili kufurahi na watoto hao katika siku
Bi.
Janet Sosthenes Mwenda akijaribu na kununua moja ya bidhaa za mikono
zinazotengenezwa na watoto wa kituo cha Kiwohede. Kushoto Mratibu
Mipango wa Kituo hicho Bi. Stella Mwambenja.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo cha
Kiwohede Bi. Justa Mwaituka akizungumza na Mtangazaji wa Kipindi cha
Ongea na Janet pamoja Crew nzima inayotengeneza kipindi hicho kuhusiana
na maendeleo yaliyokwisha fikiwa mpaka sasa na mipango ya baadae ya
kuboresha mazingira ya kituo hicho.
Mtangazaji wa kipindi cha
Ongea na Janet na crew yake wakiimbia na kufurahi pamoja na watoto wa
kituo cha Kiwohede siku ya Valentines.
Mkurugenzi Mkuu wa kituo hicho akitambulisha wageni kwa watoto wanaolelewa kituoni hapo.
Mmoja
wa watoto wanaolelewa na kituo hapo akitoa shukrani kwa Bi. Janet
Sosthenes Mwenda pamoja na Crew kwa kuonyesha upendo wa dhati kitu
ambacho ni adimu kwao kutokana na mazingira waliyotoka.
Mtangazaji
wa Kipindi cha Ongea na Janet akizungumza na watoto wa kituo cha
Kiwohede ambapo amewataka kudumisha upendo baina yao na kujiona kama
watu wengine, pia amewaasa kukazania elimu ambayo itawakomboa na kuweza
kuwa kama yeye hapo baadae na amewaahidi kuendelea kuwa nao pamoja.
Janet
Sosthenes Mwenda na Crew nzima ya Ongea na Janet wakikabidhi msaada wa
fedha taslim Shilingi laki 5 kwa mwakilishi wa watoto hao ikiwa ni
upendo wake katika siku hii ya wapendanao.
Baadhi ya Watoto wa kituo cha Kiwohede wakifurahia msaada huo kutoka kwa kipindi cha Ongea na Janet.
Crew nzima ya Ongea na Janet katika picha ya pamoja na watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Kiwohede.
Janet Sosthenes Mwenda akishow love na Mkurugenzi Mkuu wa shirikila lisilo la kiserikali la Kiwohede Bi. Justa Mwaituka.
SOURCE; BONGO CELEBRITY
No comments:
Post a Comment