 |
| Kansela Angela Merkel na Rais Obama |
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameanza ziara nchini Marekani
ambako amekutana na rais wa nchi hiyo, Barack Obama. Agenda ya
mazungumzo yao itajikita zaidi katika mzozo wa Ukraine unaofukuta
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameanza ziara tarehe 01.05.2014 nchini
Marekani ambako anatarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo, Barack
Obama. Katika ziara yake hiyo iliyoanza jana itajikita kuongelea mzozo wa
Ukraine unaofukuta utasaidia kufifisha kashfa ya kunaswa mawasiliano ya
simu na kansela huyo kulikofanywa na shirika la usalama wa kitafa la
Marekani, NSA.
Wakati uhusiano kati ya Urusi na mataifa tajiri ya magharibi haujawahi
kuwa mbaya kama ulivyo tangu vita baridi, viongozi wa siasa na wataalamu
wafikiria kuwa mzozo wa Ukraine utawafanya kuwa na msimamo mmoja baada
ya miezi 6 ya mkwaruzano.
Hoja zitakazo jadiliwa na viongozi hao wawili ni mkakati wa kumshinikiza
rais Vladimir Putin wa Urusi, na mkataba wa ushirikiano katika nchi za
magharibi ambao umekuwa ukijadiliwa kati ya marekani na Jumuia ya Umoja
wa Ulaya, alisema mshauri wa Kansela Merkel
Hii ni ziara ya kwanza ya bi Angela Merkel Washington tangu aliye kuwa
mfanyakazi wa idara ya upelelezi ya Marekani Edward Snowden kutangaza
kuwa kituo cha uchunguzi wa data za eletroniki cha Marekani, kimekuwa
kikinasa mawasiliano ya simu Ujerumani na hususan simu ya kiganjani ya
kansela.