Thursday, May 1, 2014

COURTNEY KOTEWA AWA MSHINDI WA SHINDANO LA "SHARE THE EXPERIENCE PHOTO"


(Picha hiyo ya juu imepigwa na Eric  Magayne)Shindano la Share the Experience photo contest limefanyika na picha iliyoshinda na kutangazwa leo ni picha iliyopigwa na mwanadada Courtney Kotewa ndani ya hifadhi ya ya taifa ya Lakeshore huko Michigani na kushinda dola 10,000. lakini picha iliyoongezewa ubunifu  ni picha iliyopigwa katika ukingo wa Ziwa Powell katika hifadhi inayoitwa Glen Canyon National Recreation Area.Picha hiyo inamuonesha mtalii akitembea katika ukingo hatari katika sehemu hiyo huko Utah, Staggs amefanya hivyo katika wakati ulio sawa akaongeza na ubunifu wake akampiga picha mtalii akitembea pembeni ya bwawa (pool) akaunganisha na sehemu ya ukingo wa Lake Powell Glen Canyon National Recreation Area. Picha hiyo ilikuwa katika shindano hilo la Share the experience photo contest 2013 ikiwa ni kati ya picha 18,000 zilizowakilishwa kwa ajili ya shindano hilo lililodhaminiwa na National Park Foundation. Picha nyingine ziangalie chini ni nzuri sana kutazama……

Picha iliyopigwa na Peter Blanchard
Picha ilipigwa na Linnea Charnholm
Picha ya Darell Staggs


Picha iliyoshinda ya mwanadada Courtney Kotewa
Picha iliyopigwa na Michal Mcruiz

Picha iliyopigwa na Graham McGeorge

No comments:

Post a Comment