Katibu mkuu wa
chama cha Mapinduzi, komredi ABDULRAHMAN KINANA amewataka wananchi kuwa makini
dhidi ya wanasiasa wanaopita mitaani na kudai kuwa upatikanaji wa katiba mpya
ndio suluhu ya matatizo yao.
Amesema
kauli mbalimbali zinazoendelea kutolewa na baadhi ya wanasiasa nchini kuhusiana
na suala la muungano na muundo wa Serikali tatu ndani ya katiba ijayo, zina
lengo la kutaka kujilimbikizia madaraka na vyeo ambavyo kimsingi havina tija
kwa maslahi ya Watanzania.
Akizungumza
katika mkutano wake na wananchi wa Jimbo la BUKENE, wilaya ya NZEGA mkoani
TABORA mara baada ya kukagua miradi ya maendeleo, katibu mkuu huyo wa CCM
amesema wanasiasa hao walipokuwa katika vikao vya bunge la katiba mjini Dodoma
wameonekana kutetea maslahi yao zaidi kuliko haki za wananchi wa kawaida.
Katika hatua
nyingine Mbunge wa jimbo la Bukene SULEYMANI ZEDI alizungumza katika mkutano
huo, amesema Serikali imefanikiwa kutimiza
ahadi ya kupeleka umeme katika jimbo hilo, ingawa bado kuna changamoto kubwa ya
kukosekana kwa nguzo.
Ziara ya katibu
mkuu wa CCM, bado inaendelea mkoani Tabora ambapo baadae ataelekea mkoani
Singida kwa ajili ya kuangalia utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya chama hicho
ya mwaka 2010.
No comments:
Post a Comment