Mwanariadha anayekabiliwa na kesi ya
mauaji nchini Afrika Kusini Oscar Pistorius alikuwa na majuto baada ya kumuua
mpenzi wake.
Hii ni kwa mujibu wa ushahidi wa
jirani yake huku kesi dhidi ya mwariadha huyo ikianza kusikilizwa tena baada ya
kuahirishwa kwa wiki mbili.
Johan Stander jirani yake Oscar,
alikuwa mtu wa kwanza kuja nyumbani kwa Oscar baada ya Oscar kumpiga risasi
mpenzi wake marehemu Reeva Steenkamp mwaka jana.
Pistorius amekana madai kuwa alimuua
mpenzi wake kwa maksudi.
Anasema kuwa alifyatua risasi
kupitia mlango wa chooni wakati akiwa katika hali ya kuogopa akidhani kuwa
mwizi alikuwa amevamia nyumba yake.
Bwana Stander alitaka kuonyesha kuwa
Bwana Pistorius' alikuwa na majuto na uchungu mwingi kwa kumuua mpenzi wake na
kwa hivyo huenda alimuua kwa bahati mbaya.
"Niliona ukweli asubuhi ile na
ninahisi hivyo ndivyo ilivyokuwa,’’ Sanders aliambia mahakama."Alitaka
sana kumuokoa na alichofanya tu ni kumuomba Mungu,’’ aliongeza kusema shahidi
huyo.
Stander, anayeishi umbali wa mita
350 kutoka nyumbani kwa Oscar, aliitwa nyumbani kwa Oscar punde baada ya mauaji
hayo.
Alisema kuwa mwanariadha huyo
alimwambia kwamba: ''Nimemuua Reeva nikidhani alikuwa jambazi kavamia nyumba
yangu, tafadhali njoo haraka.’’
Bwana Stander alisema kuwa
alipowasili nyumbani kwake Oscar alimuona mwanaridha huyo akishuka ngazi akiwa
amembeba Reeva.
"Alikuwa analia, akipiga
mayowe, akiomba Mungu,’’ alisema Stander naye akiwa analia.
‘‘Sidhani ni kitu ningependa kuona
tena maishani mwangu,’’ alisema jirani huyo
Stander aliambia mahakama kuwa eneo
hilo lilikuwa limewahi kuvamiwa , ingawa kwa ujumla wake ni mahali salama.
No comments:
Post a Comment