Shirika lisilo la kiserikali linalowasaidia
wazee wilayani Karagwe (SAWAKA) limeanza kutekeleza mikakati yake yenye
lengo la kupunguza kasi ya vitendo vya ukatili na manyanayaso dhidi ya
wazee wanayokumbana nayo katika jamii.
Akizungumza wakati wa warsha maalumu
iliyoandaliwa na shirika hilo Mkurugenzi Mtendaji wa SAWAKA LIVINGSTONE
BYEKWASO amesema shirika limeanza kuwawezesha wazee kiuchumi ili waweze
kujiongezea kipato.
Nao baadhi ya wanahabari waliohudhuria
warsha hiyo akiwemo LILIAN LUGAKINGIRA, MBEKI MBEKI na AGNES DAMAS kwa nyakati
tofauti wameishauri serikali kubuni mikakati mbalimbali itakayochangia
kukomesha kabisa vitendo vya ukatili na manyanyaso wanayokumbana nayo
wazee.
Tangu lianzishwe shirika hilo mwaka 2005
limeshawajengea wazee nyumba zaidi ya MIA MBILI TISINI na MOJA.
No comments:
Post a Comment