Tuesday, May 6, 2014

UKWELI KUHUSU MKATABA WA WAYNE ROONEY KUBAKI MANCHESTER UNITED



Mkataba wa Wayne Rooney wa sasa hivi unaonyesha anachukua mkwanja mrefu sana wa paundi 250,000 kwa wiki. Baada ya kuomba uhamisho mwaka 2010 , Manchester United ilimfanya Rooney kuwa mchezaji anayelipwa pesa nyingi duniani, wakati wanampa mkataba mpya kwa kumfanya abaki kwenye klabu hiyo. 

Kwa hatari ya kukosa Klabu bingwa Ulaya wameonyesha nia ya kumbakiza Rooney klabuni hapo na mkataba mpya mzuri wa paundi 300,000 kwa wiki. Ongezeko hilo la paundi 50,000 kwa wiki inaweza isionekane kubwa kwa pato la wachezaji maarufu lakini kupata paundi 300,000 kwa wiki ni kitu ambacho hatujawahi kuona mchezaji akilipwa.

No comments:

Post a Comment