Walimu na wadau wa elimu mkoani Mbeya wameitaka
Serikali kutoa elimu kwa jamii juu ya mpango wa matokeo makubwa BRN ili mpango
huo uweze kuleta tija.
Wakizungumza katika hafla ya kukabidhi
vyeti kwa shule ambazo zimeongeza ufaulu kwenye mitihani ya kitaifa mkoani
Mbeya, baadhi ya walimu wamesema bado kuna changamoto kubwa ya jamii kutoelewa
malengo ya mpango huo,kiasi cha baadhi ya wazazi kutotoa ushirikiano katika
maendeleo ya taaluma kwa watoto wao.
Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro amesema suala la maendeleo ya taaluma mkoani Mbeya
ni jukumu la jamii nzima, hivyo ni muhimu kwa wazazi na walimu kushirikiana
katika kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora
Mkoa wa Mbeya ni miongoni mwa mikoa ambayo
imefanya vizuri kitaaluma katika mwaka wa masomo wa 2013/2014 ukishika nafasi
ya tatu katika mikoa yote ya Tanzania bara sambamba na kutoa shule iliyoongoza
kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne mwaka 2013.
No comments:
Post a Comment