Serikali imetakiwa kuweka mipango ya matumizi bora ya
ardhi kwa kutenga maeneo ya wakulima na wafugaji ili kuepusha migogoro ya mara
kwa mara ya wakulima na wafugaji, ambayo imekuwa ikisababisha vifo vya wananchi
na mifugo katika maeneo mbalimbali nchini.
Rai hiyo imetolewa na Kamati ya Bunge ya kilimo,
mifugo na maji kupitia kwa mwakilishi wake AMINA MAKILAGI na Kambi Rasmi ya
upinzani bungeni kupitia kwa Waziri Kivuli wa Mifugo na Uvuvi ROSEMARY KAMILI
wakati wakitoa maoni kwa makadirio ya mapato na matumizi ya wizara ya Mifugo na
Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2014/2015.
Pamoja na rai, suala na kuiwezesha sekta ya mifugo
kuchangia pato la Taifa limezungumziwa, huku Kambi rasmi ya upinzani bungeni
ikitaka kuwasilishwa bungeni kwa taarifa ya uchunguzi ya kamati ya Ardhi,
Maliasili na Mazingira kuhusu migogoro ya wakulima, wafugaji na hifadhi, huku
wakitaka kufutwa kwa kodi ya mifugo.
Awali akiwasilisha hotuba ya makadirio ya bajeti ya
Wizara yake kwa mwaka 2014/2015 suala la oparesheni tokomeza, waziri wa Mifugo
na Uvuvi Dk. TITUS KAMANI ameahidi kutenga maeneo maalum kwa ajili ya wafugaji
ikiwa ni sehemu ya kupunguza migogoro baina ya wafugaji na watumiaji wengine wa
ardhi huku akibainisha kuwepo kwa ongezeko la uzalishaji wa nyama.
Tanzania ina jumla ya Ngombe milioni 22.8, Mbuzi
milioni 15.6, Kondoo milioni 7, Nguruwe milioni 2.01, Kuku wa Asili milioni
35.5 na Kuku wa kisasa milioni 24.5.
No comments:
Post a Comment