Wednesday, May 7, 2014

MANCHESTER CITY USO KWA USO DHIDI YA ASTON VILLA KUELEKEA KUWA BINGWA WA B.P.L MSIMU HUU

Ligi kuu ya Uingereza Barclays Premier League inatarajia kuendelea leo Jumatano 7 Mei 2014, Manchester City ataikaribisha Aston Villa ndani ya Etihad huku Man City akitakiwa kushinda mechi hiyo kwa hali na mali ili kupata pointi tatu muhimu ili afikishe pointi 83 pointi mbili mbele ya hasimu wake mkubwa katika kugombea kuchukua ubingwa wa ligi hiyo msimu huu Liverpool.

Aston Villa nae anahitaji ushindi ili aweze kuweka historia ya kuinyima na kuondoa tumaini la Man City kuwa bingwa mpaka itakapofika Jumapili 11 Mei 2014 zitakapochezwa mechi za kufunga msimu huu.Mechi nyingine itakuwa kati ya Sunderland dhidi ya West Brom,huku timu zote zikipigana ili zisishuke daraja, na mechi zote zitachezwa saa 3:45 usiku wa leo.

No comments:

Post a Comment