Vikosi vya serikali ya Sudan Kusini na waasi wanaendelea kupigana
wakivunja makubaliano mapya ya amani na kuondoa matumaini ya kumaliza
miezi mitano ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Mapigano yamepamba moto katika jimbo tajiri kwa mafuta la Nile ya
juu,kwa mujibu wa waziri wa ulinzi Kuol Mayang aliyesema vikosi vya
serikali vimeamariwa" visende kupigana,lakini vijihami tu
vikishambuliwa."
Tangu rais Silva Kiir na kiongozi wa waasi Riek Machar walipotia saini
makubaliano ya kuweka chini silaha ijumaa iliyopita,pande zote mbili
zinaendelea kulaumiana kuanzisha upya mashambulio .
"Riek Machar havidhibiti vikosi vyake na wanamgambo wake wenye silaha
nzito nzito wanaojulikana kama "Jeshi jeupe" wanaojipakaa jivu kama
alama ya vita na wakati huo huo kuepusha wasitafunwe na mbu"
wamewashambulia wanajeshi wa serikali,waziri wa ulinzi Manyang
ameendelea kusema.
"Hivi si vikosi vya kawaida,jeshi jeupe limeundwa na raia na
hawajaarifiwa chochote kuhusu makubaliano yaliyofikiwa ili kusitisha
uhasama-waziri huyo wa ulinzi wa serikali ya mjini Juba amesema na
kuongeza waasi ndio waliokuwa wa kwanza kushambulia.
Nae msemaji wa jeshi Philip Aguer amesema wasimamizi kutoka jumuia ya
IGAD wanapelekwa Bentiu,mji mkuu wa jimbo tajiri kwa mafuta Unity .
Rais Salva Kiir amesisitiza alipokuwa akiuhutubia umati wa watu huko
Juba kwamba anataka amani."Tumewaamuru wanajeshi wetu wasibanduke mahala
walipo kuwashambulia waasi."Amesema.
Pande hizi mbili ziliwahi kukubaliana kuweka chini silaha mwezi january
uliopita,lakini makubaliano hayo hayakukawia kuvunjika na wimbi jipya la
mapigano kuripuka.
Wachunguzi wa mambo wanasema pande zote mbili zinakabiliwa na changamoto
ya jinsi ya kutekeleza makubaliano ya amani huku muungano wa makundi ya
wanamgambo yakiwaleta pamoja wanajeshi walioasi na makundi
yanayohasimiana ya kikabila.
Pande zote mbili zinalaumiana kuwatumia mamluki na waasi kutoka nchi
jirani ya Sudan huku upande wa serikali ukiungwa mkono na wanajeshi wa
Uganda-Muundo wa Uongozi wa Kiir unatajikana pia kuwa dhaifu.
No comments:
Post a Comment