![]() |
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akihutibia wananchi katika uwanja wa Kibandamaiti Zanzibar. |
CHAMA cha Mapinduzi (CCM) kimemtaka Katibu Mkuu wa Chama cha
Wananchi (CUF) Seif Sharif Hamad kama kweli hataki Muungano wa serikali mbili
amuandikie barua Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Shein na kujiuzulu wadhifa wake
wa Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar.
Tamko hilo lilitolewa jana na Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana wakati akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara
uliofanyika kwenye viwanja vya Kibandamaiti mjini Unguja. Kinana alisema
anachokifanya Seif ni sawa na kuwaramba visogo wanasiasa wenzake wa upinzani,
wakati yeye akipata mshahara na marupurupu mengine yanayomwendesha maisha yak
echini ya serikali ya CCM.
Alisema kama kweli Maalim Seif anajigamba ni jasiri
achukue uamuzi sahihi wa kujiuzulu wadhifa wake ili apate nafasi ya kutosha kuwatumikia
wananchi nje ya Serikali. Kinana alieleza kuwa kutembea nchi nzima kwa Seif si
kitendo cha uungwana kufanywa na kiongozi mwenye wadhifa wa Makamu wa kwanza wa
Rais akiwa ndani ya Serikali inayompa mshahara na huduma nyingine muhimu
akaamua kuwachcochea wenzake ambao wako nje ya Serikali kuleta chokochoko dhidi
ya Serikali anayoitumikia. Maalim Seif ameshatuhumiwa kuwa kigeugeu katika
maisha yake ya kisiasa ambapo hivi karibuni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,
Mohammed Seif Khatib alielezea namna kiongozi huyo wa CUF alivyowahi kuwa
mtetezi wa serikali mbili alipokuwa kiongozi katika Serikali ya CCM ambako
alitumia nguvu kubwa kupinga vuguvugu la kudai serikali tatu mwaka 1984.Khatibu
alinukuu kauli ya Maalim Seif alipokuwa akipambana na watu waliokuwa wakaitaka
serikali tatu akiwemo Rais wa Zanzibar wakti huo Aboud Jumbe.
“Msimamo wa Jumbe
umetufadhaisha sisi sote tunataka maelezo yake kwa kuwa ni dhahiri hoja ya
serikali tatau haikuanzishwa na watu wadogo, imechangiwa pia na baadhi ya
viongozi wa Baraza la Mapinduzi na Aboud Jumbe ni chanzo cha hayo” alinukuliwa
Maalim Seif akisema mwaka 1984. Viongozi ambao Maalim Seif alisema wnataka
serikali tatu na kwa kufanya hivyo wamemfadhaisha na wanastahili adhabu pamoja
na Jumbe ni Jamal Faki, Abuu Salim na Wolfgang Dourado ambaye alikuwa
mwanasheria Mkuu wa kwanza wa Zanzibar.
“Tuangalie viongozi
wanaobadilikabadilika mwaka 1984 Maalim alitaka serikali mbili, mwaka 1992
akiwa CUF msimamo wake ukawa serikali tatu, juzi serikali ya mkataba, huyu ni
kiongozi wa aiana gani? Ni wa kuongopea watu tu”. Alisema Khatibu Aman nia
mbaya Kinana katika mkutano wa jana aliendelea kusema. “Maalim Seif aache
kuwababaisha wananchi atulie kwa sababu ameamua kutumikia serikali za CCM na
hana uwezo wowote wa kuvuruga amani ya Taifa kama anavyojigamba kwenye majukwaa
ya kisiasa.
Aliongeza kuwa Katibu Mkuu
huyo wa CUF anaposimama na kutaka muundo wa Muungano wa serikali tatu hiyo ni
danganaya toto lakini kila mwenye macho na amasikio anatambua nia ya kiongozi
huyo ni kutaka kuusambaratisha Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa maslahi
yake na rafiki zake. Kinana alisema Tanganyika kukosa Serikali wakati Zanzibar
ikiwa na mamlaka ya ndani si kioja kwani hata Uingereza yenye Muungano wa nchi
za Wales, Scotland, Ireland ya Kaskazini na England ina kiti kimoja Umoja wa
mAtaifa.
Pia alisema England ambako anatoka Malkia Elizabeth II haina serikali.
Kwa upande wake Mnadhimu wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Salmin Awadh Salmin
alisema wawakilishi wa CCM wanatazamia kuwasilisha hoja binafsi kwenye Baraza
la Wawakilishi Zanzibar ili wananchi waulizwe kama wanaafiki mfumo wa Serikali
ya Umoja wa Kitaifa visiwani humo au la. Salmin alisema dhamira na madhumuni ya
kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa imefutika na haileti tena matumaini
kwa wananchi kwa kuwa pande mbili za kisiasa zinazounda ushirika huo zina
itikadi zinazotofautiana.
No comments:
Post a Comment