Alfajiri ya Mei 21 mwaka 1996 ni siku
itakayobaki kwenye kumbukumbu ya Watanzania baada ya watu zaidi ya 800 kufariki
dunia kufuatia Meli ya MV Bukoba waliyokuwa wakisafiria kutoka mkoani Kagera
kuelekea Mwanza kuzama katika Ziwa Victoria.
Tukiadhimisha miaka 18 tangu kutokea kwa
ajali hiyo iliyokatisha maisha ya wapendwa wetu, taifa leo linakumbuka simanzi
kutokana na kupoteza ndugu, uhai wa watu hao, ikiwemo mchango wao katika
kuliletea taifa maendeleo.
Wakati ajali hiyo inatokea Rais
Mstaafu wa Awamu ya tatu BENJAMIN WILLIAM MKAPA alikuwa madarakani.
Ajali za majini zimeendelea kutokea ambapo
Septemba 10 mwaka 2011 Meli ya Spice Islander ilizama katika eneo la Nungwi
ikitokea Bandari ya Malindi Zanzibar na kuua zaidi ya watu 100.
Mwaka mmoja yaani Julai 18 2012, baadae
karibu na Pwani ya Zanzibar Meli ya MV Skagit iliyokuwa ikitokea Dar es Salaam
kwenda Zanzibar ilizama na kuua abiria 146 kati ya 290 waliokuwa kwenye meli
hiyo.
Mara nyingi binadamu hujifunza kutokana na
makosa, ambapo ajali hizi mara nyingi zinadaiwa kusababishwa na uzembe wa
baadhi ya watendaji na watoa huduma
Aidha jamii imeitakiwa kwa ujumla kuimarisha usalama katika usafiri
wa majini na sio kuiachia mamlaka husika pekee.
No comments:
Post a Comment