Chriss Brown alifungwa jela baada ya
kumpiga aliyekuwa mpenzi wake Rihana
Mwanamuziki wa Marekani Chris Brown
atasalia jela kwa siku nyingine 131 baada ya kukiri kukiuka amri ya mahakama
kuhusu kifungo cha nje alichokuwa amepewa na mahakama.
Muimbaji huyo wa muziki wa mtindo wa
R&B alikiri mahakamani mjini Los Angeles mnamo siku ya Ijumaa kuwa alitenda
uhalifu mjini Washington Oktoba mwaka jana.
Jaji alimuhukumu kifungo cha siku
365 jela ingawa alimpongeza kwa kuhudumia siku 234 katika kituo cha kupata
ushauri nasaha.
Brown amekuwa chini ya aungalizi wa
mahakama tangu mwaka 2009 alipokiri kumpiga mwanamuziki mwenza na ambaye
alikuwa mpenzi wake wakati huo,Rihanna.
Mshindi huyo wa tuzo la Grammy
amekuwa kizuizini tangu mwezi Machi alipokamatwa kwa kukiuka amri ya mahakama
iliyomweka ndani ya kituo cha ushauri nasaha pamoja na jela.
Kifungo alichopata kuongezewa siku
kinahusiana na kisa cha ugomvi kilichotokea mjini DC mwaka jana.
Brown anakabiliwa na mashitaka ya
kumchapa mwanamume mmoja nje ya hoteli moja mjini Washington
No comments:
Post a Comment