KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI |
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI JESHI LA POLISI TANZANIA.
R.P.C Ofisi ya Kamanda wa
Polisi, Mkoa wa Mbeya,
Namba ya simu 2502572 S. L. P.
260,
Fax -+255252503734 MBEYA.
E-mail:rpc.mbeya@tpf.com.tz
YAH: TAARIFA YA JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA KWA VYOMBO VYA HABARI “PRESS RELEASE”TAREHE 06.05.2014.
1. MWANAMKE WA MIAKA 70 AUAWA
NAWATU WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA SHAMBANI.
2. MZEE WA MIAKA 70 AFARIKI
DUNIA BAADA YA KUGONGWA NA GARI WILAYANI RUNGWE.
3. JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAWASHIKILIA WATU WAWILI KWA TUHUMA MBALIMBALI.
KATIKA TUKIO LA KWANZA:
MWANAMKE MMOJA ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA MESIA SHOTI (71) MKAZI WA KIJIJI CHA SISITILA ALIKUTWA
AMEBAKWA KISHA KUUAWA KWA KUPIGWA NA VITU BUTU SEHEMU ZA KICHWANI NA MTU/WATU
WASIOFAHAMIKA NA KISHA MWILI WAKE KUTUPWA SHAMBANI.
TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO
TAREHE 05.05.2014 MAJIRA YA SAA 06:00 ASUBUHI HUKO KATIKA KIJIJI
CHA SISITILA, KATA YA SISITILA, TARAFA YA IYUNGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. MWILI
WA MAREHEMU ULIKUTWA NA JERAHA SEHEMU ZA KICHWANI. CHANZO CHA TUKIO HILO BADO
KINACHUNGUZWA. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA YA
MBEYA.UCHUNGUZI ZAIDI WA TUKIO HILI BADO UNAENDELEA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WALIOHUSIKA NA TUKIO HILI AZITOE KATIKA
MAMLAKA HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA TUKIO LA PILI:
MZEE WA MIAKA 70 ALIYEFAHAMIKA
KWA JINA LA MKISU LEMBUKA MKAZI WA KAYUKI AMEFARIKI DUNIA WAKATI
ANAPATIWA MATIBABU HOSPITALI YA SERIKALI MAKANDANA –TUKUYU WILAYA YA RUNGWE
BAADA YA KUGONGWA NA GARI LISILOFAHAMIKA.
AWALI MNAMO TAREHE 04.05.2014
MAJIRA YA SAA 16:00 JIONI HUKO KATIKA KIJIJI CHA KAYUKI, KATA NA
TARAFA YA TUKUYU GARI NA DEREVA ASIYEFAHAMIKA LILIMGONGA MZEE HUYO NA
KUMSABABISHIA MAJERAHA. CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI. DEREVA AMBAYE PIA
HAKUFAHAMIKA ALIKIMBIA NA GARI MARA BAADA YA TUKIO.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO HASA KWA KUZINGATIA SHERIA NA
ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA. AIDHA
ANATOA WITO KWA WATEMBEA KWA MIGUU KUTEMBEA PEMBENI MWA BARABARA NA KUVUKA
SEHEMU ZENYE VIVUKO ILI KUEPUKA AJALI .AIDHA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE
TAARIFA ZA MAHALI ALIPO MTUHUMIWA [DEREVA] WA TUKIO HILI AZITOE KATIKA MAMLAKA
HUSIKA ILI AKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAKE.
KATIKA MISAKO:
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA
LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA NEFA LETSON (30) MFANYABIASHARA,
MKAZI WA LUPA-DARAJANI AKIWA NA POMBE KALI [VIROBA] ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA
SERIKALI AINA YA RIDDER KATONI 12 NA BOSS KATONI 01.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA
MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE 05.05.2014 MAJIRA YA SAA 15:30 ALASIRI
HUKO KATIKA KITONGOJI CHA LUPA –DARAJANI, KIJIJI CHA KIBAONI, KATA YA
CHOKAA, TARAFA YA KIWANJA, WILAYA YA CHUNYA, MKOA WA MBEYA. MTUHUMIWA NI MUUZAJI
WA POMBEHIZO. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI MTUHUMIWA ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WAFANYABIASHARA KUACHA KUUZA/KUSAMBAZA BIDHAA ZILIZOPIGWA MARUFUKU NA SERIKALI
KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA YA MTUMIAJI.
KATIKA MSAKO WA PILI, JESHI LA
POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA RAIA NA MKAZI WA NCHINI ETHIOPIA
AKIWA AMEINGIA NCHINI BILA KIBALI.
MHAMIAJI HARAMU ALIKAMATWA
KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA KATIKA ENEO LA ITEZI, KATA YA ITEZI, TARAFA YA IYUNGA
JIJI NA MKOA WA MBEYA. TARATIBU ZA KUMKABIDHI IDARA YA UHAMIAJI ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA
KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA
WANANCHI KUENDELEA KUTOA TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOWATILIA MASHAKA KATIKA MAENEO
YAO ILI WAKAMATWE NA UCHUNGUZI DHIDI YAO UFANYIKE.
Imesainiwa na:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA.
No comments:
Post a Comment