Wafanyakazi wa VETA Makete wakiwa katika picha na watoto yatima wa kituo cha Bulongwa. |
Akizungumza
na mwandishi wetu kwa niaba ya wafanyakazi wenzake alioambatana nao Bw.
Mathew Komba amesema wao kama VETA Makete wameguswa na namna watoto hao
wanavyopata tabu kwani hawakupenda kuishi maisha hayo lakini kutokana
na kufiwa na wazazi wao ndiyo maana wapo katika kituo hicho
Amesema
awali walikuwa wamepanga kuwatembelea watoto hao kabla ya pasaka lakini
kutokana na sababu zisizoepukika walishindwa kufanya hivyo lakini
walijipanga kama walivyokuwa wamedhamiria na jana walifika kituoni hapo
kuwaona watoto hao na kuwapa msaada huo
Bw.
Komba amesema baadhi ya vitu walivyovikabidhi ni pamoja na mafuta ya
kupikia, sukari, mchele, sabuni, juisi, dawa za meno na vingine vingi
vyote vikiwa na thamani ya tsh. 329,000/=
Amewaomba
wadau wengine kuwaunga mkono kwa kwenda kuwasaidia watoto yatima kwani
ni jukumu la jamii kwa ujumla kuhakikisha wanawatunza watoto hao licha
ya kwamba wanalelewa kwenye vituo mbalimbali
Kwa
upande wake Bi Sekela Nkyami kutoka kituo hicho cha kulelea watoto
yatima Bulongwa amesema ingawa kituo hicho kina vitega uchumi mbalimbali
lakini bado kinategemea misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali
wakiwemo wakazi wa Makete wenye moyo wa huruma kama walioufanya chuo cha
VETA
Amesema
watoto hao waliopo katika kituo hicho si mali ya kituo pekee bali ni wa
jamii yote kwa hiyo kuiomba jamii kushirikiana nao katika matunzo ili
watoto hao wasijisikie wapweke kutokana na uyatima walio nao
No comments:
Post a Comment