Mikoa ya MWANZA
na IRINGA bado inakabiliwa na changamoto ya wananchi wake kushindwa kutambua
dalili za awali za magonjwa yasiyopewa kipaumbele, huku zaidi ya watu bilioni
mbili wakiwa hatarini kupata maambukizi ya magonjwa hayo.
Kwa mujibu
wa ripoti na tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa maambukizi ya magonjwa
yasiyopewa kipaumbele ikiwemo usubi, matende, ngirimaji, minyoo ya tumbo,
kichocho na trakoma yametajwa kuathiri kwa kiasi kikubwa jamii maskini.
Wakizungumza
jijini Dar es Salaam, waratibu wa magonjwa hayo kutoka mikoa ya Mwanza na
Iringa wamesema elimu ya ufahamu wa dalili za mapema za maradhi hayo
inahitajika kutolewa hasa ikizingatiwa kuwa athari zake ni ulemavu wa kudumu.
Katika
kukabiliana na athari za magonjwa hayo Serikali kupitia wizara ya Afya na
ustawi wa Jamii imekuwa ikipanga mikakati mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha
wananchi wanakuwa na uelewa wa kutosha.
No comments:
Post a Comment