Sunday, May 11, 2014

MANCHESTER CITY BINGWA MPYA WA LIGI KUU YA UINGEREZA 2013/14

Ligi kuu ya Uingereza imemalizika leo kwa Manchester City kuwa bingwa mpya wa ligi hiyo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa, mpaka mwisho timu zilizokuwa zikipewa nafasi ya kuwa mabingwa Liverpool na Man City zinaingia uwanjani haikujulikana nani ni bingwa ngawa Man City alikuwa anapewa nafasi zaidi kuliko Liverpool. Manchester City leo iliikaribisha West Ham United katika uwanja wa Etihad ambapo katika dakika ya 39 Nasri aliiweka Man City na ubingwa baada ya kupiga shuti kali liligonga nguzu ya kushoto kwa chini na kuingia golini, baada ya West Ham United kuwaacha Man City kucheza mpira golini kwao huku  wao wakiwa wanazuia muda wote.

 Na goli la pili la Manchester City lilifungwa Kapteni wa timu Vicent Kompany katika dakika 49 dakika tano tu baada ya kipindi cha pili kuanza na kuiweka Man City sehemu salama katika kuwa bingwa wa Uingereza kwa mara ya pili ndani ya misimu mitatu. Baada ya kipenga cha mwisho mashabiki wa Man City waliingia uwanjani kwa furaha kuwafuata wachezaji ni kufanya uwanja wote kujaa mashabiki katika sehemu ya kuchezea (pitch). Mechi nyingine ilikuwa ni Liverpool dhidi ya Newcastle na Liverpool ameshinda 2 – 0 na kukamata nafasi yake ya pili kwa tofauti ya pointi 1 alizotofautiana na bingwa Man City mwenye pointi 86.

Mechi nyingine kwenye ligi zilizochezwa leo ni Cardiff 1 – 2 Chelsea, Fulham 2 – 2 Crystal Palace, Hull 0 – 2 Everton, Liverpool 2 – 1 Newcastle, Man City 2 – 0 West Ham United, Norwich 0 – 2 Arsenal kutokana na kufungwa kwa Norwich ndo tiketi yake ya kushuka daraja. Southampton 1 – 1 Man United, Sunderland 1 – 3 Swansea, Tottenham 3 – 0 Aston Villa na West Brom 1 – 2 Stoke. Timu nyingine zilizoshuka daraja ni Norwich na Fulham.Mfungaji bora wa ligi hiyo ni Suarez mwenye magoli 31, Sturridge 21 wote wachezaji wa Liverpool, nafasi ya tatu kwa ufungaji inashikiliwa na Yaya Toure wa Man City ana magoli 20, Aguero wa Man City na Rooney wa Man United wamelingana kwa magoli kila mmoja ana magoli 17.

No comments:

Post a Comment