Baadhi ya wananchi
wa wilaya ya Mkalama Mkoani Singida wameiomba ofisi ya usajili wa vizazi na
vifo Wilayani humo, kupunguza urasimu juu ya upatikanaji wa vyeti baada ya
malipo.
Wakiongea
kwenye mkutano wa baraza la madiwani, baadhi ya madiwani akiwemo ABDALAH
MKILYA wamesema licha ya ucheleweshaji huo, pia vinauzwa kwa gharama ya
Shilingi elfu 10 badala ya shingi elfu mbili kama ilivyoainishwa kwenye risiti.
Akijibu
malamamiko hayo, katibu tawala wa wilaya hiyo Benjamin Mwombeki amesema kiasi
cha fedha kinachotozwa sasa kipo kisheria, isipokuwa stakabadhi zinazotumika
zinaonyesha kiwango cha zamani.
Aidha
katika hatua nyingine madiwani hao wameiomba serikali ya Wilaya hiyo kutafuta
ufumbuzi wa tatizo la mipaka kati ya wilaya yao na Mbulu, Hanang, Karatu,
Iramba, na Singida vijijini, pamoja na mipaka ya ndani baina ya kata na
kata.
Halmashauri ya Wilaya Mkalama ni kati ya Wilaya mpya
nchini, zilizoanzishwa na kupata hadhi kamili ya kuwa Wilaya.
No comments:
Post a Comment