Monday, May 12, 2014

MWENYEKITI WA HALMASHAURI YA KIBAHA ATOA MUDA WA WIKI MBILI KUHAKIKISHA ZAHANATI YA GALAGALA INAFUNGULIWA

MWENYEKITI wa halmashauri ya mji wa Kibaha ADHUDADI MKOMAMBO ametoa muda wa wiki mbili kwa madiwani wa halmashauri hiyo kuhakikisha zahanati  ya galagaza iliyopo kata ya Msangani, inaanza kufanya kazi  kwa ajili ya kuwahudumia  wagonjwa.

Kauli hiyo imekuja kufuatia  hoja iliyotolewa na Diwani wa kata ya Msangani LEONARD MLOE katika kikao cha baraza la madiwani ambaye alitaka ufafanuzi kuhusu ujenzi wa zahanati hiyo  ambayo imemalizika kwa muda  mrefu lakini  haijaanza kutumika.
 Akijibu hoja hiyo,mwenyekiti huyo wa halmashauri amesema hakuna sababu yoyote ya zahanati hiyo kushindwa kuanza kufanya kazi ukizingatia  mambo yote muhimu yameshakamilika ikiwemo nyumba  ya daktari.
Hoja hiyo ya sakata la kufunguliwa kwa  zahanati imeonekana kuwakera viongozi waliohudhuria kikao hicho hali iliyomlazimu  mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi CCM Wilayani Kibaha MAULID BUNDALA kusimama na kueleza kusikitishwa na kutokufunguliwa kwa zahanati hiyo wakati ipo tayari.
Wakazi wa kata ya msangani wanalazimika kutembea umbali wa  zaidi ya kilomita 10 kufuata huduma za afya katika  kata ya mwendapole kutokana na kukosa huduma hiyo kwenye kata yao.

No comments:

Post a Comment