![]() |
Barabara kuu ya kuelekea Wilaya ya Kilolo, eneo la Ndiwili ikiwa imeharibika vibaya, na hivyo msimu huu wa mvua katika mashimo kujaa maji. |
Hayo yamezungumzwa na mkuu wa Wilaya ya
Kilolo Gerlad Guninita wakati akisoma taarifa ya utekelezaji wa
shughuli za serikali kwa kipindi cha miezi mine, kuanzia January hadi
april mwaka 2014.
Guninita amesema kushindwa kukamilika kwa barabara hizo kunachangia hali ya uchumi kudumaa, kwa kuwa mazao mengi ya kilimo na biashara katika Wilaya hiyo yanategemea kuuzwa katika masoko ya nje ya Wilaya.
Amesema kutokukamilika
kwa wakati kwa barabar hizo kumeyafanya magari yanayosafirisha mazoa na
bidhaa mbalimbali kukwama, na hivyo kudumaa kwa uchumi wa wananchi wa
Wilaya ya Kilolo.
Akitaja barabar zilizotengewa fedha Guninita amesema Wilaya ya Kilolo ilipanga kutekeleza shughuli mbalimbali za ujenzi, huku ikitenga jumla ya shilingi Bilioni moja, miamoja
sitini na sita, laki tisa na elfu mbili (1, 196, 902, 000/= ambazo
zingetumika kwa ujenzi wa miradi ya barabara kwa kipindi cha 2013/2014.
Guninita amesema fedha hizo
zilidhamilia kukamilisha jumla ya miradi 12 ya ukarabati na ujenzi wa
barabara, katika maeneo mbalimbali, yakiwemo matengenezo ya barabara ya
Idete- Kiwalamo, yenye urefu wa km 16, ujenzi uliotengewa zaidi ya
shilingi 367.
Ametaja ujenzi wa daraja la Kiwalamo,
ujenzi wa Lami katika barabara ya Ilula mjini, ambayo itagharimu zaidi
ya shilingi Milioni 363, huku matengenezo ya barabara ya Ruaha Mbuyuni-
Msosa yenye km 6, ambayo ujenzi wake unaendelea na zaidi ya shilingi
Milioni 53 zilielekezwa katika kazi hiyo.
Ujenzi wa barabara ya Ibumu – Ilambo, Ilula- Image km
16.5 iliyopangiwa kiasi cha shilingi Milioni 107, pamoja na ukarabati
wa barabara ya Kilolo mjini, Kitowo – Mwatasi na Kilolo- Nguruhe
iliyotengewa kiasi cha shilingi Milioni 101.
Pia amesema kuna ukarabati wa barabara
ya Ihimbo- Kising’a, Wotalisoli-Udekwa, Makungu- Mlafu km 23 fedha
zilizopangwa zikiwa ni zaidi ya shilingi Milioni 105, na barabara
nyingine kama ya Ilula mjini- Vitono, Uhambingeto na Kipaduka- Ikuka
12.5 fedha zaidi ya shilingi milioni 108, na kazi inaendelea.
Amezungumzia matengenezo ya barabara ya
Kidabaga- Bomalang’ombe, Ukumbi- Masege, mawambala- Winome na
Bomalang’ombe- Mwatasi km 26 na kiasi cha fedha zilizoidhinishwa kwa
ujenzi huo zikiwa ni shilingi Milioni 94.
Aidha amesema kuna matengenezo ya
barabara ya Mtandika – Nyazwa, Mtandika – Msosa, Mahenge- Irindi- Magana
na Irole- Kitumbuka zenye km 27 kwa kiasi cha shilingi Milioni 206,
660,000/=.
Maeneo mengine yaliyopangiwa fedha kwa
ajili ya ukarabati wa barabara ni Mwatasi- Ng’ungula na Ng’ingula-
madege km 23 kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 209, huku barabara ya
Idete- Mhanga na ujenzi wa daraja la Mhanga kwa kiwango cha fedha kiasi
cha shilingi Milioni 209, 291, 000/=.
Hata hivyo muhandisi wa Halmashauri ya
Wilaya hiyo ya Kilolo amesema mpango wa kufanikisha ujenzi huo ni kutoa
tenda kwa wakandarasi kuanzia mwezi wa saba ili kutokwamisha na hali ya
jiografia ya Wilaya hiyo.
"Wilaya ya Kilolo kama inavyofahamika
jografia yake niya mvua kwa msimu mrefu, kwa hiyo ili kufanikisha ujenzi
wa barabar zetu tutakuwa tunatoa kazi kwa wakandarasi msimu ambao mvua
zimemalizika kunyesha," alisema.
No comments:
Post a Comment