Mahakana ya Kimataifa ya Uhalifu ya mjini The Hague Uholanzi imemuhukumu
mbambe wa kivita kutoka Congo, Germain Katanga, miaka 12 gerezani baada
ya kukutwa na hatia ya kuwapa silaha kundi la waasi 2003 na kufanya
mauwaji.
"Mahakama imemuhukumu Germain Katanga kifungo cha miaka 12 gerezani,"
alisema Jaji Mkuu Bruno Cotte mbele ya mahakama ya The Hague ikiwa ni
hukumu yake ya pili tangu kufunguliwa kwake mwaka 2003. Jaji huyo
amesema kile kipindi cha miaka saba ambacho mtuhumiwa amekutimia akiwa
kizuizini kitapunguzwa katika miaka ya kifungo chake.
Mwezi Machi mwaka huu, Katanga mwenye umri wa miaka 36, alikutwa na
hatia ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinaadamu, yakiwemo
mauwaji na uporaji kutokana na jukumu lake katika harakati za kuvamia
kijiji cha Bogoro katika eneo tete la mashariki mwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo tarehe 24 Februari 2003.
Wakati ikitangazwa hukumu hiyo, Katanga ambaye anajulikana kwa jina
la utani la Simba, hakuonesha mtikisiko wowote mahakamani hapo.
Inaelezwa kuwa matukio hayo ya uhalifu yalifanyika wakati akiwa na umri
wa miaka 24.
Jaji aligundua kuwa alilipa silaha kundi la wapiganaji la Patriotic
Resistance Forces la mjini Ituri (FRPI) ambalo liliuwa idadi kubwa ya
watu, ikikadiriwa kuzidi 200. Jaji Cotte ameiambia mahakama ya ICC
kwamba makovu ya mapigano ya Februari 24, 2003 yameendelea kuonekana
mpaka leo hii. Amesema kutumika kwa mapanga katika mashambulizia hayo
ilikuwa vitendo vya kikatali sana na kwamba kumesababisha maumivu
yaliyokithiri.
Hata hivyo, awali mahaka ya uhalifu wa kivita ICC ilimfutia mashitaka
Katanga ya ubakaji, utumwa wa kingongo, na kutumia watoto wenye umri
mdogo jeshini. Baada ya kutolewa hukumu hiyo wanasheria kutoka kwa
upande wa Katanga watakuwa na siku 30 ya kukataa rufaa kufuatia hatua
hiyo. Hata hivyo uhamuzi rufaa hiyo bado haujatolewa.
Hukumu hio ni ya pili kutolewa tangu kufunguliwa milango ya mahakama
hiyo mwaka 2003, nyingine ilikuwa ya mbambe wa kivita ambae kwa wakati
fulani alikuwa hasimu wake Thomas Lubanga ambae mwaka Julai 2012
alihukumiwa miaka 14 gerezani.
No comments:
Post a Comment