Klabu ya Manchester United imemteua Lous Van Gaal kuwa kocha
wake mpya atakayechukua nafasi baada ya David Moyes kutimuliwa kwa miezi 10 tu.
Mholanzi huyo amesaini mkataba wa miaka mitatau na ataanza majukumu Old
Trafford msimu unaokuja ikiwa ni baada kuongoza timu ya nchi yake Uholanzi
katika kombe la dunia litakalofanyika nchini Brazil. Msaidi wa Van Gaal atakuwa
Ryna Giggs mkongwe wa klabu hiyo ambayo alitwa majukumu ya kuiongoza Man U
baada ya Moyes kufukuzwa zikiwa zimebaki mechi tatu msimu kukamilika. Van Gaal
mwenye umri wa mika 62 amewahi kuzifundisha klabu za Ajax (Uholanzi), Barcelona
(Uhispania) na Bayrn Munich (Ujerumani) ambazo aliziwezesha kushinda mataji ya
Ligi Kuu kabla ya kuajiriwa kuiona kikosi cha taifa cha Uholanzi maarufu kama “Orange”.
Kocha huyo anategemewa kufufua matumaini ya United baada ya
klabu hiyo kumaliza ya saba msimu huu chini ya Moyes na kuandikisha historia ya
kuwa na msimu mbaya zaidi kwa kipindi cha miaka 24. Van Gaal alishinda mataji
mawili ya La Liga akiwa na Barcelona na kujiunga na Bayern aliyotwaa nayo kombe
la German Cup na kufika fainali Uefa. Alijizolea umaarufu mwaka 1995 baada ya
kukiongoza kikosi kichanga cha Ajax kilichokuwa na Clarence Seadoff, Patrick
Kluivert na wengine na kutwa kombe la Uefa kwa kuilaza AC Milan ya Italia.
No comments:
Post a Comment