Serikali imetakiwa kukamilisha taratibu zote
muhimu, ikiwemo kuifanyia marekebisho sheria ya uchaguzi wa Serikali za mitaa,
ili kuepusha dosari zilizojitokeza katika uchaguzi uliopita.
Rai hiyo imetolewa na kiongozi wa Kambi Rasmi
ya Upinzani bungeni FREEMAN MBOWE, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa
hapo kwa Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ambaye amesema, hatua iliyoanza ni
maandalizi ya bajeti huku taratibu zikifanyika, kuangalia maeneo yote muhimu
yakiwemo yanayolalamikiwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Mbunge wa Kilwa MURTAZA MANGUNGU amemtaka
Waziri Mkuu kuingilia kati, mkanganyiko wa uongozi katika jiji la Dar es Salaam
kuhusu suala la uchafu uliokithiri jijini humo, kunakotokana na Halmashauri
kuacha baadhi ya majukumu kwa kisingizio kuwa ni jukumu la jiji, jambo ambalo
Waziri Mkuu MIZENGO PINDA ameshauri lianzie katika ngazi ya chini.
No comments:
Post a Comment