Chama mapinduzi CCM kimedai kufadhaishwa na
utendaji mbovu wa watendaji wa Serikali katika baadhi ya Halmashauri nchini.
Kimesema utendaji huo mbovu ni pamoja na
kutowawajibisha kwa manufaa ya umma, kama ilivyokua enzi za utawala wa hayati
mwalimu JULIUS KAMBARAGE NYERERE na mwenzake AMANI ABEID KARUME.
Akihitimisha ziara ya siku 11 mkoani
TABORA katibu mkuu wa CCM, ABDULRAHMAN KINANA, amesema mateso wanayopata
wananchi hivi sasa yametokana na baadhi ya viongozi wa Serikali kutojali
kuwatumikia wananchi huku wakiikandamiza dhana nzima ya utawala bora.
Kwa Upande wake katibu wa NEC itikadi na
Uenezi NAPE NNAUYE amedai kushangazwa na hoja za baadhi ya makundi ya wanasiasa
yanayodai kuwa ziara za katibu mkuu wa chama hicho zimelenga kuzungumzia suala
la katiba pamoja na Ukawa.
Katibu mkuu huyo wa CCM, mara baada ya
kuhitimisha ziara yake mkoani Tabora,ameelekea Singida kuangalia kero na
matatizo ya wananchi ikiwa ni muendelezo wa ziara yake.
No comments:
Post a Comment