Bunge la Tanzania hatimaye limeridhia kuzivunja kanuni
zake
ilizojiwekea katika kuendesha vikao mbalimbali ili
kuwezesha
kukamilisha kwa wakati mchakato wa mkutano wa Bunge la
Bajeti ya Serikali mwaka 2014/2015 unaotarajiwa kumalizika June 27 mwaka huu.
Mabadiliko
hayo yanayogusa ratiba ya kuanza na kuahirishwa kwa vikao kila vinapoketi
kuanzia hii leo, inaweza kuwa mwiba kwa wabunge wasioweza kutumia muda
ipasavyo, kufuatia kupunguzwa dakika za kuchangia huku Siku ya Jumamosi
ikitajwa kama siku rasmi ya mkutano tofauti na awali.
Akitangaza mabadiliko hayo Bungeni Mjini Dodoma,
Mkurugenzi wa Shughuli za Bunge JOHN JOEL, amesema Kamati ya Uongozi imefikia
makubalino hayo ili kufidia muda uliopotea na hatimaye bajeti ipitishwe na
kuanza kutumika ifikapo Julai Mosi mwaka huu.
Bunge hilo limeanza kuanza vikao vyake leo na
mabadiliko hayo ya kanuni za Bunge pia yanatoa fursa kwa kila Wizara
kuwasilisha Bajeti ya Makadirio ya Mapato na Matumizi yake kwa kipindi cha siku
moja tu na muda utaongezwa mara itakapotokea dharura.
No comments:
Post a Comment