Imeelezwa kuwa wanawake wakiwemo
wajane ni miongoni mwa makundi ambayo yamekuwa yakiangaliwa na jamii, katika
kuhakikisha yanapata fursa mbalimbali zinazojitokeza, huku kukiwa na changamoto
ya makundi hayo kutojitambua katika kufuatilia na kuzitumia fursa hizo.
Hali hiyo inachangiwa na wanawake
wajane walio wengi kujiona wanyonge katika jamii, lakini kupitia mashirika
mbalimbali ,vikundi na serikali kwa ujumla, jitihada mbalimbali zimefanywa
ikiwemo kutoa elimu ili kuhakikisha kundi hilo linapata fursa sawa hasa katika
upatikanaji wa mikopo.
Akizungumza Afisa Mtendaji wa
kata ya uwanja wa Taifa Manispaa ya Morogoro Bi. ANNA KOBERO amesema, kwa
kipindi kilichopita kina mama wa kata hiyo wamekuwa na tatizo la kupata mikopo,
lakini tangu kuanzishwa kwa vikundi vya kuweka na kukopa, kina mama wengi
wameweza kujikwamua kiuchumi na kukabiliana na umaskini na
unyanyasaji wa kipato.
Bw. SALUM KURUGE na Bi. ZAWADI
CHANZI ni baadhi ya wanachama wa kikundi cha UMOJA VICOBA cha kata ya
Uwanja wa Taifa, ambao wamesema kupitia kikundi hicho, kujikopesha wao kwa wao
imekuwa ni faida kubwa.
Kikundi cha Umoja Group cha kata ya Uwanja
wa taifa manispaa ya Morogoro kilianzishwa mnamo mwaka elfumbili na kumi na
tatu na kina wanachama thelathini.
mwisho
No comments:
Post a Comment