ZAIDI ya wananchi
200 wa Kijiji cha Utaho jana wamefanya maombi kwenye eneo la ajali
lililosababisha vifo vya watu 19, baada ya kugongwa na basi la Sumry, barabara
kuu ya Singida-Dodoma.
Katika ibada
hiyo, Wananchi wakiongozwa na viongozi wao wa dini Padri Felix Mange, mchungaji
wa kanisa la Pentekoste Francis Pius na imamu wa kijiji hicho Haruna Senga
wameiasa jamii kuchukua tahadhari wanapotumia barabara hiyo.Baada ya maombi
hayo baadhi ya wakazi wa mji wa singida wameeleza kusikitishwa na ajali hiyo na
wameiomba jamii kuendelea kuwafariji wale wote waliopoteza ndugu zao.
April 28 mwaka
huu watu 19 walipoteza maisha wakiwemo askari polisi wanne,viongozi watatu wa
kijiji na wengine wanane kujeruhiwa, baada ya kugongwa na basi la Sumry kwenye
eneo la Utaho, Mkoani Singida.
No comments:
Post a Comment