Baada ya miaka nane kupita bila Arsenal (The Gunners)
kupata kikombe chochote, Leo hii Jumamosi 17
Mei 2014 wamefanikiwa kuchukua
kikombe cha ubingwa wa FA kwa kuicharaza 3 – 2 Hull City katika mchezo uliokuwa
mkali sana na wa kusisimua huku timu zote zikipelekeshana.
Hull City ndio waliokuwa wa kwanza
kuliona lango la Arsenal mapema kabisa katika dakika ya 4 kwa goli lililofungwa na Chester na dakika
nne baadae katika dakika ya nane Davies aliipatia Hull City goli la pili.
Goli
la Kwanza la Arsenal lililorudisha matumaini lilifungwa katika dakika ya 17 na
Carzola na mpaka inafika mapumziko ilikuwa Arsenal 1, Hull city 2. Katika
kipindi cha pili dakika ya 71 Koscielny aliwainua mashabiki wa Arsenal baada ya
kupachika goli wavumi.
Dakika za kawaida zilimalizika zikaongezwa
nyingine 30 na dakika 15 ziliisha bila timu yeyote kuliona lango la mwenzake.
Katika kipindi cha pili katika muda wa nyongeza dakika ya 109 Ramsey alipachika
goli zuri lilipea jina la Arsenal classic goal of the match baada ya kupewa
pasi kwa kisigino na bila kutuliza Ramsey akanyoosha golini na kuiandikia
Arsenal goli la 3 na ndilo lililowapa ushindi wa FA 2014. Imekuwa ni furaha kwa
mashabikiwa Arsenal, kocha na wachezaji kwani ni muda mrefu miaka nane Arsenal
hakushinda kombe lolote.
No comments:
Post a Comment