Ukosefu wa elimu ya mahesabu ya kisasa juu
ya ufungaji, uwasilishaji na utoaji taarifa za fedha kwa halmashauri
nyingi hapa nchini inaelezwa kuwa kiwazo kwa halmashauri hizo kufikia
malengo ikiwa ni pamoja na kupata hati chafu.
Mtaalamu wa masuala ya Fedha kutoka
kampuni ya Better Business Consultant ya Jijiji Dar es salaam PEACE
LUMELEZI,amebainisha hayo wakati akitoa mafunzo maalumu juu ya ufungaji
wa mahesabu kwa wahasibu wa serikali kutoka halmashauri za wilaya ya
Kigoma na kuongeza kuwa hali hiyo inakwamisha juhudi za kujiletea
maendeleo katika baadhi ya halmashauri nchini.
Mpaka sasa zaidi ya watu 600 nchini kutoka Taasisi za
serikali na binafsi wamekwisha nufaika na mafunzo hayo yanayolenga kuongeza
kasi ya utendaji kazi kwa wahasibu.
No comments:
Post a Comment