Uhaba wa wauguzi nchini unasababisha wauguzi
kuhudumia wagonjwa wengi kinyume na mwongozo wa shirika la afya duniani
unaoelekeza muuguzi mmoja kuhudumia wagonjwa kati ya sita hadi wanane kwa siku.
Hali hiyo imejitokeza pia katika wilaya ya
Momba mkoani Mbeya ambapo muuguzi mmoja anahudumia wastan wa wagonjwa 30 hadi
40 kwa siku.
Akisoma risala kwa niaba ya
wauguzi,muuguzi DORIS JAPHET amesema tatizo la uhaba wa wauguzi linapelekea
wafanye kazi kupita uwezo wao hali inayosababisha kutoa huduma chini ya
kiwango.
Nao baadhi ya wadau wa afya wilayani momba
wamesema mbali na tatizo la uhaba wa wauguzi, pia vituo vya kutolea huduma za
afya havitoshelezi.
No comments:
Post a Comment