 |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kashikana mikono na viongozi wa
serikali na wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA)
huku wakiimba wimbo wa wafanyakazi katika kilele cha Siku ya
Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014 katika Uwanja wa Taifa
jijini Dar es Salaam. (picha: IKULU) |
Rais Jakaya
Kikwete, amewaahidi wafanyakazi nchini kuwa mambo mazuri yakiwemo ya
kupanda kwa mishahara na kupunguzwa kwa kodi ya mishahara maarufu kama
P.A.Y.E.
Akihutubia kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Dar es Salaam leo, Rais Kikwete amesema:
“Najua hiki ndio kilio chenu na wote mnasubiria kwa
hamu Serikali inasema nini? Nawaahidi kuwa katika hotuba ya Bajeti
Waziri wa Kazi na Ajira, itabainisha wazi, kiwango cha mshahara ambacho
Serikali imekiongeza katika mishahara ya wafanyakazi,” alisema Rais
Kikwete.
 |
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipungia mkono waandamanaji aliowapokea
katika kilele cha Siku ya Wafanyakazi Duniani (MEI MOSI) leo Mei 1, 2014
katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. |
 |
Rais Kikwete akizungumza na wafanyakazi katika sherehe za Mei Mosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.Rais Kikwete, alisema Serikali haitoweza kupandisha mishahara hiyo na
kufikia ombi la Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA), la Sh
750,000.
Pamoja na hayo, Rais Kikwete alionyesha kutoridhishwa na namna sehemu
kubwa ya sekta binafsi, isivyozingatia viwango vya mishahara
vinavyopangwa na Serikali, hali inayochangia kuibuka kwa migogoro ya
mara kwa mara baina ya waajiri na waajiriwa.
Akizungumzia suala la Kodi ya Mapato (P.A.Y.E), Rais Kikwete, alisema
ombi hilo nalo kama ilivyo nyongeza ya mishahara ni la muda mrefu, na
kuwaahidi wafanyakazi hao kuwa nalo linafanyiwa kazi ili kupunguza
kutoka asilimia 13 inayotozwa kwa sasa na kufikia tarakimu moja.
Naye Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudentia Kabaka, alimpongeza Rais Kikwete
kwa kupatiwa tuzo ya utawala bora Afrika, na kuwataka waajiri nchini
kutumia fursa hiyo kumuenzi kiongozi hiyo kwa kuhakikisha wanafuata
nyayo na kusimamia utawala bora, ili kupunguza migogoro ya kazi.
Katibu Mkuu wa Tucta, Nicholaus Mgaya, akiwasilisha risala ya
wafanyakazi katika maadhimisho hayo, aliiomba Serikali ishughulikie
matatizo yanayowakabili wafanyakazi ya uboreshaji wa mishahara,
kupunguzwa kwa kodi ya P.A.Y.E na kuboreshewe pensheni.Taarifa zinasema kuwa
maadhimisho hayo maarufu kama Mei Mosi yameingia dosari baada ya mmoja
wa wafanyakazi kufariki dunia uwanjani kwa ghafla akiwa katika
maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam.
Mfanyakazi huyo anayedaiwa kufanya kazi Ikulu alizidiwa ghafla akiwa
katika maandamano na kupatiwa huduma za kwanza lakini hali yake ilizidi
kuwa mbaya na hatimaye kudaiwa kupoteza maisha wakati akipatiwa huduma
na madaktari na wahudumu kutoka kikosi cha msalaba mwekundu waliyokuwa
katika maadhimisho hayo.
Mfanyakazi huyo aliletwa katika kambi ya watu
wa huduma ya kwanza iliyokuwa katikati ya uwanja wa Uhuru, kisha
kupatiwa huduma ya kwanza bila mafanikio na baadaye alifariki dunia. Kwa
mujibu wa taarifa kutoka katika kundi ambalo lilimleta mfanyakazi huyo
baada ya kuzidiwa ghafla lilimtaja kuwa jina lake ni Rashid John
Chilwangwa.Mmoja wa wafanyakazi waliyokuwa wameandamana na mfanyakazi huyo
ambaye hakupenda kutaja jina lake kwa kuwa yeye si msemaji akisimulia
tukio hilo, alisema John Chilwangwa (45) walikuwa naye katika sherehe za
maadhimisho na hali yake ilibadilika kabla ya kuingia uwanjani na
aliomba aende kujisaidia haja ndogo baada ya hapo alianza kuishiwa
nguvu.
“…Si tulishangaa alikaa muda kidogo akijisaidia baada ya kumfuata
tulimkuta ametoka ndani ya choo na kuja nje na kisha kukaa kwenye tofali
huku akisema anajisikia kuishiwa nguvu na hali ilibadilika ndo
tukamleta hapa,” alisema shuhuda huyo.
Alipoulizwa hali yake kwa sasa ambapo alikuwa ameingizwa kwenye hema la
huduma ya kwanza kwa wahudumu kutoka kikosi cha msalaba na madaktari
alisema wamejaribu kumuhudumia lakini bahati mbaya amefariki dunia
tayari.
“…Tumeambiwa na madaktari kuwa ameshafariki tayari,” alisema shuhuda huyo ambaye alikuja na mgonjwa huyo.
Mwandishi wa habari hizi alishuhudia madaktari wakijaribu kumtundikia
dripu huku wakijaribu kurudisha mapigo ya moyo kwa kushtua mara kadhaa
lakini juhudi ambazo hazikuzaa matunda. Baada ya kubaini amefariki dunia
walisita kumwekea dripu ambayo ilikuwa inaandaliwa na badaye
walimfunika kwa shuka nyeupe na kuita gari la wagonjwa tayari kwa
kumpeleka hospitali kwa uchunguzi zaidi. Hata hivyo hakupatikana mara
moja daktari kuzungumzia kilichomsibu Chilwangwa.
Baadhi ya jamaa aliyoambatana nao wakimwangalia mara baada ya kufikishwa chumba cha huduma ya kwanza. (picha: The Habari)
Rais Kikwete akifurahia jambo katika sherehe za Mei Mosi jijini Dar es salaam
Wafanyakazi.
Mibingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2014 Azam FC wakipita mbele ya Rais Kikwete kwenye sherehe za Mei Mosi Alhamisi 1 Mei 2014 katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam.
| | |
|
|
|
No comments:
Post a Comment