Saturday, May 3, 2014

MASTAA WAMUUNGA MKONO DANI ALVES KUPINGA UBAGUZI KWA KUPIGA PICHA WAKILA NDIZI

Dani Alves akila ndizi aliyorushiwa na shabiki.
Mastaa wengi duniani wameonekana kumsupport mwanasoka kutoka Brazil kwa kula ndizi baada ya mchzaji huyo kutupiwa ndizi wikiendi iliyoisha huko Hispania katika mechi moja ya ligi kuu ya nchi hiyo La Liga kitendo hicho kikimaanisha ubaguzi wa rangi kwa kumuona mchezaji huyo mweusi kama yeye ni nyani. Baada ya kurushiwa ndizi Dani Alves kabla ya kupiga kona akaifuata ndizi akaiokota akaimenya na kuila na kisha kupiga kona hiyo, kitendo hichi kimetazamwa kama ni cha kishujaa kwani amekubali yeye ni mtu mweusi na kama wanamuona yeye ni nyani basi sawa. Shabiki huyo aliyetupa ndizi hiyo amefungiwa kuingia katika mechi za timu yake maisha yake yote. Katika kumsupport Dani Alves mastaa wengi duniani wamepost picha wakiwa wanakula ndizi na hawa ni baadhi ya mastaa hao akiwemo mwanamuziki Davido kutoka Nigeria.
Davido (kulia)
Etoo
Baloteli (kulia juu) Suarez na Neymar (kulia chini)
Kocha wa timu ya Italia Cesare Prandelli na kiongozi huko nchini Italia.

No comments:

Post a Comment