 |
Suarez akilia huku akiwa amefunika uso |
The Crook Liverpool wameshindwa kuonyesha umwamba wao katika kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza jana kwa kubali sare ya 3 - 3 dhidi ya timu ya Crystal Palace. Mpaka dakika ya 78 Livepool walikuwa wkiongoza 3 - 0 kwa magoli yaliyofungwa na Allen katika dakika ya 18, Sturridge dakika ya 53 na Suareza dakika ya 55. Crystal Palace walianza kuja juu baada ya kufanya mabadiliko na kuingia Gayle, Crystal Palace katika dakika ya 79 walipata goli kupitia kwa Delaney na goli lingine lilifungwa na Gayle katika dakika 81 na lingine akifunga huyo huyo Gayle katika dakika ya 88, nakufanya matokeo kuwa 3 - 3 mpaka mwisho. Liverpool amefikisha pointi 81 baada ya kugawana pointi moja moja na Crystal Palace. Baada ya mechi kuisha Suarez alianza kulia huku akiwa ameficha uso wake na jezi mpaka anaingia chumba cha kubadilishia nguo.
Mechi nyingine ni leo wakati Man United anaivaa Hull akiwa Old Trafford chini ya Giggs. Na kesho Man City ambae amerudisha matumaini ya kuwania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza kesho anakutana na Aston Villa na mechi nyingine itakuwa kati ya Sunderland Vs West Brom. Liverpool anaongoza ligi akiwa mbele kwa pointi moja dhdi ya Man City mwenye pointi 80 na nafasi ya tatu inashikiliwa na Chelsea yenye pointi 79, nafasi ya nne inashikiliwa na Arsenal yenye pointi 76 na nafasi ya tano inashikiliwa na Everton mwenye pointi 69.
No comments:
Post a Comment