Thursday, May 8, 2014

ANC YAONGOZA UCHAGUZI WA KIHISTORIA ULIOFANYIKA JANA

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC) kinaongoza katika uchaguzi wa kihistoria uliofanyika Jana.
Maafisa wa tume ya uchaguzi wamesema kuwa baada ya hesabu ya matokeo ya awali ya nusu ya kura zilizopigwa, ANC imejizolea takriban asilimia 60 ya kura zilizohesabiwa .

Chama cha upinzani cha Democratic Alliance, kinashikilia nafasi ya pili kwa asilimia 24 ya kura, ikiashiria ongezeko maradufu ya kura ikilinganishwa na uchaguzi uliotangulia.

Chama kipya kinachoongozwa na aliyekuwa kiongozi wa tawi la vijana katika ANC JULIUS MALEMA, kinashikilia nafasi ya tatu na asilimia 5 ya kura zilizopigwa

No comments:

Post a Comment