Mhadhiri mwandamizi wa shule ya uandishi wa habari Dk. Ayou Rioba |
Pamoja na wakuu wa nchi nyingi
duniani kusaini mkataba wa uhuru wa vyombo vya habari, bado sheria za nchi
nyingi zinakinzana na mkataba huo, ikiwemo sheria ya magazeti ya mwaka
1976 ambayo inatumika hapa nchini.
Akizungumza katika maadhimisho ya
siku ya uhuru wa vyombo vya habari, yanayofanyika kitaifa jijini Arusha,
mhadhiri mwandamizi wa shule ya uandishi wa habari Dk. AYOUB RIOBA
amesema, sekta ya habari imepiga hatua licha ya changamoto nyingi
zinazoikabili.
Naye mwanahabari mwandamizi LEILA
SHEHE amewataka waandishi wa habari kujitathmini katika uhuru huo, ili kuona
kama unatekelezwa hasa kwa kutoa habari kwa kuheshimu misingi yake.
Baadhi ya waadhishi wa habari
akiwemo mhadhiri mwandamizi wa chuo kikuu cha Iringa SIMON BEREGE,
wameitaka serikali kuweka sheria dhidi ya wanaotumia mitandao vibaya, ili
kila mtu aweze kuitumia.
Mkutano huo wenye kaulimbiu ya ‘’uhuru
wa vyombo vya habari kwa utawala bora na maendeleo’’ umewakutanisha
waandishi wa habari kutoka ndani na nje ya nchi, ambapo leo wamiliki wa
vyombo vya habari, wanatarajiwa kuungana nao katika kujadili changamoto
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment