Taarifa za hivi punde ni kwamba mwandishi absalom kibanda aliyekuwa akishitakiwa kwa kesi ya uchochezi ameshinda kesi.
Mbali na Kibanda, washtakiwa wengine walikuwa ni Meneja Uendeshaji Biashara
wa Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, Theophile Makunga na
mwandishi wa safu ya Kalamu ya Mwigamba katika gazeti la Tanzania Daima,
Samson Mwigamba amabo nao wameachiwa huru..Makala hiyo iliyodaiwa kuwa ya uchochezi ilikuwa na kichwani cha
habari kisemacho; “Waraka maalumu kwa askari wote” ambayo ilichapishwa
Novemba 30, 2011.