Friday, May 2, 2014

LIPULI NA HARAKATI ZA KUPANDA LIGI KUU

CHAMA cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Iringa (IRFA) kimesema tmu ya soka ya Lipuli imepata bahati ya mtende ambayo kama itatumiwa vyema itacheza Ligi Kuu msimu ujao.
“TFF imeamua kuongeza timu mbili zitakazopanda daraja, moja kati yake itatoka katika timu tatu zilizoshika nafasi ya pili kwenye makundi matatu yaliyomaliza ligi daraja la kwanza hivikaribuni,” alisema Katibu wa IRFA, Elliud Mvella.

Mvella amesema Lipuli ni moja kati ya timu hizo zitakazoshiriki Ligi ndogo ya tatu bora mjini Dodoma ili kupata mshindi atakayepanda daraja.
Naye Mwenyekiti wa IRFA, Cyprian Kuyava amewaomba wadau wapenda mchezo huo kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali ili ijiandea vyema kwa ligi hiyo.
“Ni fursa, fursa muhimu, kama tutaitumia vyema basi hakuna shaka kwamba msimu ujao, wakazi wa Iringa wataona Ligi Kuu,” alisema

No comments:

Post a Comment