Imeelezwa kuwa
mvua zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo hapa nchini zinazidi
kuleta madhara kwa wananchi wa Wilaya ya Kibaha, Mkoani Pwani kutokana na
kuharibu miundombinu ya barabara, umeme, vyoo pamoja na kuathiri kwa
kiasi kikubwa utendaji wa kazi zao.
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti, baadhi ya wananchi hao akiwemo ABDALLAH SIMBA na
KASSIM YAHAHA wamesema, madhara ya mvua hizo yamesababisha maisha yao
kuwa magumu.
Aidha wananchi
hao wametoa wito kwa serikali kulitafutia ufumbuzi suala hilo, kwa kuhakikisha
wanajipanga vilivyo katika kuiboresha miundombinu ya barabara na kufanya
ukarabati wa madaraja.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Pwani HAJAT MWANTUMU MAHIZA, ametoa tahadhari kwa
wananchi kuwa makini hasa kwa wale wanaoishi katika maeneo ya mabondeni na wale
wanaotumia vyombo vya baharini.
Mvua hizo
zinazoendelea kunyesha katika baadhi ya maeneo zimesababisha uharibifu mkubwa
wa miundombinu ya barabara, kuharibika kwa nguzo za umeme, upotevu wa mifugo
pamoja na kubomoka kwa baadhi ya madaraja madogo ambayo yalikuwa
yamejengwa chini ya kiwango.
No comments:
Post a Comment