Praslin ni kisiwa cha pili kwa ukubwa huko Seychelles, kina wakaazi wanaofikia 6,500. Zamani kilitumiwa na wafanyabiashara wa Uarabuni na maharamia wakati wa safari zao kwenye bahari ya Hindi, kwa sasa ni mashuhuri kwa shughuli za utalii, pamoja na hoteli nzuri za kitalii pia fukwe zake zenye mchanga mweupe wa baharini ni vivutio vikubwa kwa watalii, baadhi ni pamoja na fukwe za Anse Lazio na Anse Georgette ambazo ni fukwe nzuri sana Duniani.
2. ZANZIBAR:
Kisiwa cha Unguja ni kisiwa kikubwa huko Zanzibar na chenye wakaazi wengi zaidi ya kisiwa cha Pemba, pembezoni mwa pwani ya Tanzania. Zanzibar palikuwa ni sehemu muhimu sana kwa biashara ukanda huu wa Afrika Mashariki, kulikuwa na mchanganyiko wa Waafrika, Wahindi na Waarabu. Kivutio kikubwa cha Zanzibar ni Mji Mkongwe (Stone Town), kivutio kingine ni fukwe zenye mchanga mweupe wa baharini.
3. MAURITIUS:
Mauritius ni kisiwa kidogo kilichopo bahari ya Hindi, mashariki ya Madagascar na kusini mashariki ya seychelles. Kisiwa cha Mauritius kilikuwa hakikaliwi na mtu hadi mwaka 1598 Wadachi walipoingia kisiwani humo, Wadachi walishindwa kuvumilia hali ya hewa hapo na mwaka 1710 walikikimbia kisiwa hicho. Wafaransa walikuja kuhamia baada ya miaka mitano toka Wadachi kuhama, Wafaransa walikaa kisiwani hapo hadi waliponyang'anywa na Waingereza mwaka 1810 na kukiita kisiwa hicho Mauritius. Mauritius ina fukwe nzuri na za kuvutia.4. KISIWA CHA LAMU - KENYA:
Kisiwa cha Lamu kipo Kenya kwenye bahari ya Hindi, ni kisiwa chenye historia ya muda mrefu ya Waswahili na tamaduni ya Kiswahili katika Afrika ya Mashariki, kisiwani Lamu hakuna mabarabara makubwa ila njia nyembamba za magari na vichochoro vya waenda kwa miguu na baiskeli. Lamu ni kisiwa chenye magari machache sana.
5. REUNION:
Reunion ni kisiwa kilichokuwa chini ya uangalizi wa Wafaransa, kikiwa na idadi ya watu wapatao 800,000, mashariki ya Madagascar na kusini magharibi ya Mauritius, kisiwa ambacho mabaharia wa kutoka Afrika, Uarabuni na Ureno walikuwa wakikitumia sana wakati wa safari zao baharini. Reunion inaweza kufananishwa na visiwa vya Hawaii kijiografia kwa tabia za sura ya nchi zinavyofanana.
No comments:
Post a Comment