Mbu aina ya Aides anaeambukiza homa ya dengu. |
Kufuatia
kuongezeka kwa idadi ya wagonjwa wa Homa ya Dengu katika jiji la Dar es Salaam,
Serikali imeendelea kutoa elimu kwa watendaji wa sekta ya afya na wananchi kwa
ujumla, ili waweze kujikinga na ugonjwa huo, pamoja na kunyunyizia dawa kwenye
maeneo yenye mazalia mengi ya mbu.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. KEBWE STEVEN KEBWE amesema, pamoja na
kuchukuliwa kwa hatua hizo pia Serikali kupitia Bohari Kuu ya Madawa (MSD),
imejipanga kuagiza dawa za kutosha kwa ajili ya kutibu maradhi nyemelezi na
kufanyia vipimo vya homa hiyo ambayo imezua hofu kwa jamii.
Akitoa
tamko kuhusu homa ya Dengi bungeni, kufuatia kuombwa kwa taarifa hiyo na mbunge
wa Kigamboni Dk. FAUSTIN NDUGULILE, Naibu Waziri wa Afya amesema mpaka sasa
jumla ya wagonjwa 15 bado wamelazwa, wakiwemo sita Hospitali ya Temeke, Sita
Hospitali ya Amana na Wanne Hospitali ya Mwananyamala, huku jumla ya watu 458
wakiwa wameugua homa hiyo jijini Dar es Salaam tangu kuanza kwake ambapo watatu
kati yao wamefariki.
Mbali na
Tanzania Naibu Waziri KEBWE amesema, nchi zilizopo kwenye ukanda wa joto mara
nyingi hukumbwa na homa hiyo, ambapo hivi sasa Kenya na Msumbiji pia
wanakabiliwa na Homa ya Dengu.
No comments:
Post a Comment