Kufuatia
kuwepo kwa mfululizo wa matukio ya milipuko ya mabomu katika baadhi ya nchi za
jumuiya ya Afrika mashariki hasa katika kipindi cha hivi karibuni, wananchi wa
ukanda huo wametakiwa kushiriki kikamilifu kupiga vita ugaidi badala ya
kuziachia serikali za nchi husika pekee.
Rai
hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati ya mahusiano na utatuzi wa migogoro
katika ukanda wa Afrika mashariki Abubakari Zein katika mkutano
unaojadili hali ya amani na utatuzi wa migogoro, ambayo katika kipindi hiki
matukio ya kigaidi yameelezwa kuongezeka.
Nchi
ya Kenya imeshuhudia matukio kadhaa ya milipuko inayodaiwa kuhusishwa na ugaidi.
Washiriki
kutoka pande mbali mbali za Afrika mashariki wamehudhuria mkutano huo akiwemo Benard
Murunya kutoka Tanzania ambae anabainisha kuwa mkutano huo ni muhimu
kutokana na matukio yanayoendelea katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki.
Mkutano
huo umewakutanisha wabunge wa bunge la Afrika mashariki lengo
likiwa ni kujadili hali ya usalama na matukio ya kigaidi yanayoendelea
kushamiri ambapo mwaka jana mlipuko mkubwa katika jengo la biashara la WESTGET
nchini Kenya uliuwa watu wapatao 67.
No comments:
Post a Comment