Sunday, May 4, 2014

MJUE BINADAMU MREFU ZAIDI DUNIANI ALIE HAI

Sultan Kosen
Sultan Kosen alizaliwa tarehe 10 Desemba 1982 nchini Uturuki, yeye ni mkulima ambaye anashikilia rekodi ya Dunia ya mtu mrefu zaidi aliye hai, urefu wake ni futi nane na inchi tatu (8ft 3in).
Urefu wake umemsababishia atembee kwa msaada wa gongo la kutembelea. Wazazi wake Kosen na ndugu zake wana urefu wa kawaida tu, alishindwa kumaliza shule kwa ajili ya urefu wake. Licha ya urefu wake mwenyewe anafurahia maisha yake na hupendelea kucheza gemu kwenye kompyuta na rafiki zake. 
Akizungumzia faida na hasara za urefu wake alisema kwa upande wa faida ni kuweza kusaidia familia yake kwa mambo madogo madogo kama kubadili taa, mapazia n.k. bila kutumia meza ndogo au kiti kupandia. Upande wa hasara ni kukosa saizi yake ya nguo na viatu madukani na kushindwa kupanda magari madogo ya kawaida. Kosen ana mke ambaye walioana mwezi Oktoba 2013.
Sultan Kosen akiwa na mtu wa saizi ya kawaida
mwenye urefu wa 5'8"
Sultan Kosen akiwa na binadamu aliyewahi kushika rekodi ya ufupi. He Pingping aliyekuwa na urefu wa 2'5",
He Pingping alifariki mwaka 2010.



No comments:

Post a Comment