![]() |
Kansela Angela Merkel na Rais Obama |
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ameanza ziara tarehe 01.05.2014 nchini Marekani ambako anatarajiwa kukutana na rais wa nchi hiyo, Barack Obama. Katika ziara yake hiyo iliyoanza jana itajikita kuongelea mzozo wa Ukraine unaofukuta utasaidia kufifisha kashfa ya kunaswa mawasiliano ya simu na kansela huyo kulikofanywa na shirika la usalama wa kitafa la Marekani, NSA.
Wakati uhusiano kati ya Urusi na mataifa tajiri ya magharibi haujawahi kuwa mbaya kama ulivyo tangu vita baridi, viongozi wa siasa na wataalamu wafikiria kuwa mzozo wa Ukraine utawafanya kuwa na msimamo mmoja baada ya miezi 6 ya mkwaruzano.
Hoja zitakazo jadiliwa na viongozi hao wawili ni mkakati wa kumshinikiza rais Vladimir Putin wa Urusi, na mkataba wa ushirikiano katika nchi za magharibi ambao umekuwa ukijadiliwa kati ya marekani na Jumuia ya Umoja wa Ulaya, alisema mshauri wa Kansela Merkel
Hii ni ziara ya kwanza ya bi Angela Merkel Washington tangu aliye kuwa mfanyakazi wa idara ya upelelezi ya Marekani Edward Snowden kutangaza kuwa kituo cha uchunguzi wa data za eletroniki cha Marekani, kimekuwa kikinasa mawasiliano ya simu Ujerumani na hususan simu ya kiganjani ya kansela.
No comments:
Post a Comment