Malcom Glazer aliyehinda tenda ya utata ya
kuichukua Manchester United mwaka 2005 amefariki dunia jana akiwa na umri wa
miaka 85. Mfanyabiashara huyo wa Marekani atakumbukwa kama bilionea wa Florida
aliyeichukua kuimiliki United miaka tisa iliyopita na kuwekeza zaidi ya pauni
milioni 500, Glazer mkubwa amekuwa mgonjwa kwa muda sasa na kuwaachia shughuli
za uendeshaji wa United watoto wake wa kiume, Joel na Avran.
Msemaji wa Manchester United: “fikra za kila
mmoja katika United zipo kwa familia usiku” Familia ya Glazer bado wanamiliki
Tampa Bay Buccaneers, timu ya mpira wa miguu ya Marekani waliyoinunua mwaka
1995.
No comments:
Post a Comment