Kwa muda mrefu jiji
la Dar es Salaam limekuwa likikabiliwa na msongamano mkubwa wa magari
yanayosababisha watu kuchelewa katika majukumu yao au kulazimika kuamka mapema
kutokana na kutumia muda mwingi barabarani.
Kufuatia hali
hiyo serikali imetenga kiasi cha shilingi milioni 28 elfu 945 nukta 00 kwa
mwaka wa fedha 2014/2015 ili kukabiliana na changamoto hizo.
Akiwasilisha
makadirio ya mapato na matumizi kwa Wizara ya Ujenzi Waziri wa Ujenzi Dk. JOHN
POMBE MAGUFULI, amesema fedha hizo zitatumika kujenga barabara za mchepuo
ambazo zitatumiwa kupunguza msongamano huo.
Kwa upande wa Kamati ya Miundombinu, mwakilishi wa
kamati hiyo ABDALLAH MTUTURA ameitaka wizara ya ujenzi kutenga fedha nyingi za
ndani kwa miradi ya barabara, huku Waziri kivuli wa Ujenzi FELIX MKOSAMALI
akishauri kuanzishwa kwa wakala wa barabara za vijijini ili kuongeza usimamizi.
ZARINA MADABIDA mbunge wa viti maalum,MOSES MACHALI
mbunge wa kasulu mjini, na ABDULKHARIM SHAA mbunge wa mafia, ni miongoni mwa
wabunge waliochangia hoja ya bajeti ya wizara ya ujenzi.
No comments:
Post a Comment