Ligi kuu ya Uingereza iliendelea tena wikiendi iliyoisha,
ikiwa imefikia sehemu tamu kweli kweli katika kugombea ubingwa wa ligi hiyo
maarufu duniani, huku pakiwa na ushindani mkubwa mpaka zinabaki mechi mbili
mbili lakini bado haijulikani nani hasa atachukua kombe hilo huku timu zote zikihitaji
ushindi bila kufungwa.
Timu itakayokubali kufungwa katika mechi hizi za mwisho basi atakuwa anaondoa matumaini ya kuchukua ubingwa wa Barclays Premier League msimu huu. Jana Arsenal katika kutetea kubaki top 4 na kucheza Klabu bingwa Ulaya kampeni yake ilienda vizuri baada ya kuicharaza West Brom 1 – 0, Chelsea nae alivutwa shati na Norwich nakutoka sare tasa ya 0 – 0 ni mbaya ya Chelsea katika kuwania ubingwa kwa kupoteza pointi 3 muhimu wakati ligi ikielekea ukingoni. Juzi Jumamosi West Ham iliicharaza Tottenham 2 – 0, Aston Vila ikailaza Hull 3 – 1, Man United nae sikio la kufa halisiki dawa akalazwa 1 – 0 dhidi ya Sunderland.
Newcastle nayo ikailaza 3 – 0 Cardiff, Stoke wakiibuka na ushindi mnene wa magoli 4 – 1 dhidi ya Fullham, Swansea akilazwa 1 – 0 Southampton na Everton akikubali kipigo akiwa nyumbani kutoka kwa Man City kwa magoli 3 – 2. Leo itapigwa mechi kati ya Crystal Palace dhidi ya Liverpool ikiwa ni mechi muhimu kwa Liverpool kuchukua pointi 3 na ikiwezekana kuwafunga magoli mengi ili kupunguza hatari ya kumpa ubingwa Man City kwa tofauti ya magoli. Kesho Jumanne 6 Mei 2014 zitagongwa mechi kati Man City Vs Aston Villa, Sundrland Vs West Brom. Na Jumapili 11 Mei zitachezwa mechi za mwisho itakuwa Cardiff Vs Chelsea, Fulham Vs Crystal Palace, Hull Vs Everton, Liverpool Vs Newcastle, Man City Vs West Ham, Norwich Vs Arsenal, Southampton Vs Man United, Sunderland Vs Swansea, TottenHam Vs Asto Vila na West Brom Vs Stoke.
Msimamo wa ligi kwa sasa anaongoza Man City kwa pointi 80, nafasi ya pili inashikiliwa na Liverpool akiwa na pointi 80 anazidiwa magoli 9, nafasi ya 3 inashikiliwa na Cheslea akiwa na pointi 79, nafai ya nne inashikiliwa na Arsenal yenye pointi 76 na nafasi ya tano inashikiliwa na Everton yenye pointi 69. Nafasi ya sita ni Tottenham yenye pointi 66, nafsi ya saba ni Man United yenye pointi 60, nafasi ya 8 ni Southampton yenye pointi 55, nafasi ya 9 ni Newcastle yenye pointi 49 na nafasi ya kumi ni Stoke 47.

No comments:
Post a Comment