Dereva boda boda wakiwa wamelala juu ya boda boda zao wakisubiri abiria jijini Dar es salaam. |
Mnamo Machi 10 mwaka huu operesheni
ya kukamata waendesha Pikipiki zenye magurudumu mawili maarufu kama bodaboda na
zile zenye magurudumu matatu maarufu kama bajaji, ilianza kwa wale wanaokiuka
agizo la kutoingia katika eneo la katikati ya Jiji (CBD).
Hadi kufikia Machi 20 mwaka huu,
bodaboda na bajaji zipatazo 1,679 zilikamatwa kwa makosa mbalimbali ya
kisheria, ambapo kufuatia hatua hiyo baadhi ya Wafanyabiashara wa usafiri
huo jijini humo wameeleza kuwa soko la usafiri huo kwa sasa limeyumba kwa
kiasi kikubwa.
Aidha wafanyabishara wametoa kilio
chao kwa sababu ya kushuka kwa mapato yao ya kila siku, baada ya
kuzuiliwa kusafirisha abiria kuelekea katikati ya Jiji.
Kwa upande wa Wajasiriamali
waliokuwa wakitegemea usafiri huo, kilio chao kimekuwa ni kushindwa kufikisha
bidhaa zao kwa wakati , katika maeneo yao ya biashara ambayo yapo katikati ya
Jiji.
No comments:
Post a Comment