Friday, May 2, 2014
LEO NDO HISTORIA CONCERT YA LADY JAY DEE
May 2, 2014 ndo siku ambayo historia inawekwa tena katika Historia Concert ya diva wa muziki Tanzania wa kizazi kipya Comando, Binti Machozi Mama Some Food Lady Jay Dee a.k.a Chuma cha sauti Tanzania. Historia Concert inafanyika leo usiku kuanzia saa 2 usiku till late pale katika parking ya magari ya Nyumbani Lounge kwa kiingilio cha shilingi 20,000 kwa wale wanaopenda kucheza kwa sana na shilingi 50,000/=Tsh kwa V.I.P ikiwa ni pamoja na dinner na wine mezani. Tiketi zinapatikana Nyumbani Lounge penyewe, Shear Illusion Mlimani City na Milion Hairs Salon. Kwa bookings piga simu namba 0787 630 459. Watu mnakaribishwa kushuhudia ngoma zote kali za Lady Jay Dee zikicharazwa na Machozi Band Live kuanzia Machozi, Siku Hazigandi, Distance, Yahaya mpaka Nasimama. Karibuni wote kumpa support Lady Jay Dee "Comando".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment