Jitihada za
Serikali na asasi za kiraia katika kuelimisha watu wa jamii ya ufugaji kutumia
mifugo yao kupunguza umasikini, utunzaji wa mazingira na migogoro ya ardhi,
zimeanza kuonesha mafanikio kwa baadhi ya maeneo hapa nchini.
Hali hiyo
imebainika wilaya ya Manyoni mkoani Singida baada ya baadhi ya wafugaji katika
eneo hilo, kuanza kuuza sehemu ya mifugo yao na kupata fedha zinazowasaidia
kujenga makazi bora ya kuishi na kuwapatia elimu watoto wao.
Wakizungumza
katika kijiji cha HEKA mara baada ya kutembelewa na katibu mkuu wa CCM
ABDULRAHMAN KINANA, wafugaji hao wamesema hapo awali jamii hiyo ilikuwa nyuma
kimaendeleo kwa kuwa hawakuelimishwa umuhimu wa kutumia mifugo katika
kujikwamua kiuchumi.
Kwa upande wake
katibu mkuu wa CCM komredi ABDULRAHMAN KINANA, amesema hatua hiyo imeonesha
njia kwa wafugaji ambao wanajilimbikizia mifugo na kuwa watumwa wa mifugo yao.
Mkoa wa Singida
una jumla ya wilaya tano na halmashauri zipatazo 6, huku asilimia 70 ya
wananchi wake wakitegemea zaidi shughuli za kilimo na Ufugaji kwa ajili ya
maendeleo yao.
No comments:
Post a Comment